Miss Grand Beatrice: “Kuwa single kuna faida zake”

DAR ES SALAAM: Beatrice Alex ambaye ni Miss Grand Tanzania 2025, amesema kwa sasa yupo single na hajawa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa takribani miaka miwili.
Mrembo huyo amesema mara ya mwisho kuwa na mpenzi ilikuwa mwaka 2024 kabla ya kuanza mwaka 2025, na tangu hapo ameendelea kuwa peke yake huku akiweka nguvu zaidi kwenye maandalizi na shughuli zake binafsi.
Akizungumza kuhusu hali yake ya mahusiano, Beatrice amesema wakati mwingine kuwa single kunampa uhuru wa kufanya mambo yake bila vikwazo.
“No, toka nimeanza kujiandaa, I think kabla ya last Christmas ya 2024 kuingia 2025, I was single,” amesema Miss Grand Tanzania 2025.
Aidha, amesema maisha ya kuwa single yana faida zake kwani humsaidia kupata muda wa kujitambua, kufanya kazi zake kwa uhuru na kujiwekea mipango yake binafsi bila usumbufu



