Mastaa

Miriam Mauki amlilia MC Pilipili

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Injili, Miriam Mauki, ametoa ushuhuda wake kuhusu marehemu Emanuel “Mc Pilipili”, akimuelezea kama kijana aliyekuwa na kiwango cha juu cha heshima, shukrani na hekima sifa ambazo amesema hazipatikani kwa vijana wengi wa kizazi cha sasa.

Akizungumza kuhusu maisha na tabia za mchekeshaji huyo, Miriam amesema kuwa siri kubwa ya mafanikio ya Mc Pilipili ilikuwa ni heshima na moyo wa kujua kushukuru.

“Moja ya sifa ya Emanuel ni shukrani, kitu ambacho madogo kibao wa sasa hawana hiyo tabia. Mwamba alikuwa anajua kukumbuka fadhila,” amesema.

Miriam ameongeza kuwa tofauti na vijana wengi wa siku hizi, Mc Pilipili alikuwa mtu asiyeisahau fadhila—hata kwa mambo madogo.

“Kuna madogo ambao hata ukimpeleka uwanja wa ndege, ndiyo imeishia hapo.

Hakwambii kama ndege imeondoka au bado yuko uwanjani, mpaka leo huambiwi kama alifika au aliishia stendi,” amesema akionesha jinsi Mc Pilipili alivyokuwa tofauti.
Akiendelea kusimulia, Miriam amesema:

“Yaani atakutafuta akiwa na uhitaji, na utamuona tena akiwa na uhitaji.”

Kwa huzuni kubwa, Miriam amemalizia kwa kusema:“Tumepoteza mtu mwenye heshima, upendo na hekima kwa watu wote.”

Related Articles

Back to top button