Filamu

Vince Gill atunukiwa Tuzo ya Lifetime Achievement Award

NASHVILLE: MWANAMUZIKI mkongwe wa country, Vince Gill, ameandikisha sura mpya katika safari yake ya zaidi ya nusu karne baada ya kuheshimiwa kwa kupewa tuzo ya Willie Nelson Lifetime Achievement Award katika Tuzo za CMA 2025.

Gill alipokea tuzo hiyo jana Jumatano, Novemba 19, kwenye sherehe zilizofanyika Nashville.

Kabla ya kupokea heshima hiyo, Brandi Carlile na Patty Loveless waliigusa mioyo ya mashabiki kwa onesho la muziki lililowekwa maalum kwa ajili yake, wakitumbuiza wimbo wake maarufu ‘When I Call Your Name,’ kama ilivyoripoti Variety.

Tuzo hii ya mafanikio ya maisha ilianzishwa mwaka 2012, na imeshawahi kutolewa kwa wanamuziki wenye majina makubwa katikaa muziki wa country akiwemo Kenny Rogers, Dolly Parton, Charley Pride, Loretta Lynn, Alan Jackson, na mwaka uliopita, George Strait.

Gill, mwenye miaka 68, alitambulishwa na mshindi wa mwaka uliopita, George Strait.
Baada ya kupokea tuzo, Gill alianza kwa utani, akisema alikuwa na uhakika kabisa kuwa ndiye mshindi pekee wa tuzo hiyo ambaye hajawahi kuvuta bangi.

Utani huo uliweka ukumbi kwenye hali ya kicheko kabla ya Gill kurejea kwenye hisia za heshima na shukrani, akimzungumzia Willie Nelson kama rafiki wa miaka 50 mtu ambaye, kwa maneno yake, ‘amebaki kuwa mfano wa wazi na wa upendo kwa familia.’

Safari ya maisha na shukrani kwa waliomsaidia
Kutoka hapo, Gill alitumia muda kutaja makundi mbalimbali yaliyomkuza kimuziki na kumpa nafasi aliyonayo leo.

Alimaliza hotuba kwa maneno ya upendo kwa mke wake, mwimbaji Amy Grant, akimtaja kama nafsi yenye upole mwingi kuliko yoyote aliyowahi kukutana nayo.

Related Articles

Back to top button