Ligi Kuu

Amina Kyando apigwa ‘benchi’ NBCPL

DAR ES SALAAM: MWAMUZI wa kati, Amina Kyando kutoka Morogoro na mwamuzi msaidizi namba mbili , Abdalah Bakenga kutoka Kigoma, wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB), wameondolewa kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu na kushindwa kuchukua hatua kwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria za mpira katika mechi namba 040 ya Pamba Jiji dhidi ya Singida Black Stars waliotoka sare ya bao 1-1.

Pamoja na matukio mengine, waamuzi hao walishindwa kutafsiri sheria katika tukio la kipa wa klabu ya Singida Black Stars kudaka mpira akiwa nje ya eneo la penati, hivyo kutotoa adhabu yoyote kwa kipa huyo.

Waamuzi hao pia walionekana kutetereka na kutojiamini hata katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika mchezo huo.

Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.6 & 1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button