
BAADA ya kuhitimisha safari ya Yanga kutofungwa mechi 49 za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, klabu ya Ihefu leo imelewa sukari baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Kagara Sugar katika mfululizo ligi hiy kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Novemba 29 Ihefu ilipata sifa kutoka kwa baadhi ya wapenzi wa soka kwa kuifunga Yanga 2-1 na kuhitimisha safari hiyo.
Bao la kwanza la Kagera Sugar limefungwa na Eric Mwijage dakika 67 kabla ya Hamis Kizza kupigilia msumamri wa mwisho dakika ya 83.

Katika mchezo mwingine wa ligi Singida Big Stars imeutumia vyema uwanja wake wa nyambani wa Liti baada ya kuipa kipigo kizito Namungo cha mabao 3-0.
Bao la kwanza la Singida BS limefungwa na Said Ndemla dakika 29, kisha Meddie Kagere kuongeza la pili dakika ya 66 na dakika za nyongeza wenyeji kuzidisha majonzi kwa Namungo baada kupachika bao la tatu kupitia Amisi Tambwe.