Ligi KuuNyumbani

Simba kuunguruma tena leo?

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendeleo leo kwa michezo mitatu Dar es Salaam, Morogoro na Mbeya huku mechi kivutio ikiwa kati ya Simba na Namungo.

Miamba ya soka Simba itakuwa mwenyeji wa Namungo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba inashika nafasi 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 baada ya michezo 10 wakati Namungo ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 10.

Katika mchezo wa mwisho wa ligi wa Simba Novemba 12 wekundu hao wa Msimbazi iliifunga Ihefu kwa bao 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mkoani Morogoro Coastal Union ni mgeni wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu uliopo Turiani.

Mtibwa Sugar ipo nafasi 7 ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 11 wakati Coastal Union ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 9.

Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya utawaka moto wakati Tanzania Prisons itakapoikaribisha Geita Gold ukiwa mchezo mwingine wa ligi leo.

Tanzania Prisons na Geita Gold zote zina pointi 14, zimecheza mechi 11 kila moja lakini Prisons inashika nafasi ya 8 huku Geita ikiwa ya 10 kutokana na tofauti ya mabao.

Related Articles

Back to top button