Burudani

Rais Samia ameipaisha sekta ya burudani

KATIKA kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya michezo na sanaa imeendelea kushamiri kwa kasi kubwa, ikionesha mafanikio makubwa katika idadi ya wasanii na fursa za kimataifa walizopata.

Takwimu zinaonesha kuwa wasanii waliopata nafasi ya kutumbuiza (show) nje ya nchi wameongezeka kutoka 122 kabla ya Rais Samia kuingia madarakani hadi kufikia wasanii 1,492 ongezeko la asilimia 730. Hili ni ongezeko kubwa linaloashiria kuimarika kwa ushawishi wa sanaa ya Tanzania kimataifa.

Aidha, jumla ya wasanii waliopata nafasi mbalimbali za kujitangaza na kufanya kazi zao imefikia 1,370, ikiwa ni ongezeko la mara 12 kutoka idadi ya awali ya wasanii 75. Hali hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato kwa wasanii binafsi na kuchangia katika pato la taifa kupitia fedha za kigeni zinazopatikana kupitia matamasha na maonesho ya kimataifa.

Pia, idadi ya wasanii wa nje waliopata kutumbuiza nchini Tanzania imeongezeka, jambo linaloonesha kwamba nchi inazidi kuwa kitovu cha sanaa na burudani kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Ukuaji huu ni ushahidi wa juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuweka mazingira bora kwa sekta ya sanaa na michezo kustawi na kutoa ajira kwa vijana wengi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button