
LONDON:MSANII Chris Brown amenyimwa dhamana na ataendelea kushikiliwa hadi kesi yake itakaposikilizwa Juni 13 katika Mahakama ya Crown ya Southwark, London. Anakabiliwa na shtaka la kusababisha madhara makubwa ya mwili baada ya kumshambulia mtayarishaji wa muziki Abe Diaw kwa chupa kwenye klabu ya usiku ya Tape, London, Februari 2023.
Diaw anadai Brown aliendelea kumshambulia hata baada ya kuanguka. Diaw alilazwa hospitali na baadaye akafungua kesi dhidi ya Brown, Live Nation, Sony, RCA Records na msanii mwingine, HoodyBaby, ambaye naye sasa anakabiliwa na shtaka sawa.
Brown alikamatwa wiki hii mjini Manchester aliporejea Uingereza, na hii inaweza kuhatarisha ziara yake ya “Breezy Bowl XX” iliyopangwa kuanza Juni 8 huko Uholanzi.
Shafii SabiihMay 20, 2025