Udhamini Simba Queens bil 1/-

TIMU ya soka ya Wanawake, Simba Queens leo imeingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na kampuni ya M-Bet wenye thamani ya shilingi bilioni moja.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa Habari Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema udhamini huo utaanza rasmi Oktoba 30 wakati Simba Queens itakapofungua dimba michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji AS FAR ya Morocco.
“Thamani ya timu yetu ya Wanawake imeongezeka ndio maana tumetafuta mdhamini wa timu hii bila kutegemea udhamini wa timu yetu kubwa ya wanaume ambayo pia inatumia udhamini wa M–Bet,” amesema Barbara.
Barbara amesema katika mkataba huo kila mwaka watakuwa wakipokea milioni 200 na anaamini utaboresha maisha ya wachezaji na kuongeza thamani zaidi.