Michezo Mingine

BMT yaitaka timu ya kriketi kupambana

DAR ES SALAAM:BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limeitaka timu ya taifa ya Kriketi ya vijana chini ya umri wa miaka 19 kupambana na kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.

Hayo yamesemwa na Ofisa Michezo wa BMT, Charles Maguzu, wakati wa kuikabidhi timu hiyo bendera tayari kwa safari ya kushiriki michuano hiyo, itakayofanyika nchini Nigeria kuanzia Ijumaa ya wiki hii.

Maguzu amesema bendera waliyopewa inawakilisha matumaini ya taifa na kwamba wanapaswa kuwakilisha nchi kwa heshima.

“Muende mkapambane, muwakilishe vizuri. Tunataka ushindi, na bendera hii ina maana mtakwenda kujitoa kwa ajili ya taifa,” amesema Maguzu.

Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania (TCA), Dk. Balakrishna Sreekumar, amewataka wachezaji kucheza kwa juhudi na kuhakikisha wanarudi na Kombe.

Timu hiyo inatarajia kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya Uganda Jumamosi kisha itacheza na wenyeji Nigeria Machi 30 na baadaye itacheza na Kenya. Katika kundi hilo mshindi mmoja atawakilisha kwenye fainali za Dunia.

Related Articles

Back to top button