2024 Tyson alirejea ulingoni na kipigo

LICHA ya kuhusishwa na kufilisika lakini haikuwa rahisi kumshawishi gwiji wa ngumi, Mike ‘Iron’ Tyson arejee ulingoni baada ya miaka 19 na miezi mitano kupita tangu gwiji huyo wa masumbwi duniani mwenye miaka 58, alipotangaza kustaafu ngumi za ushindani.
Tetesi za kurejea kwake zilianza mnamo Mei 12, 2020, alipochapisha video kwenye Instagram yake akifanya mazoezi na mwishoni mwa video hiyo, alipodokeza kurudi kwenye ngumi.
Maneno yake hayo yaliibua mapromota wengi wakihusishwa kulibeba pambano lake huku akihusishwa na kupambana na mabondi wenye majina makubwa wakiwemo waliostaafu na wanaoendelea na mchezo huo lakini haikuwa hivyo bali aliyepata nafasi ya kucheza na bingwa huyo wa miaka yote ni Jake Paul mwenye miaka 31 ambaye alifanikiwa kushinda pambano hilo lililopigwa Novemba 15, 2024 katika ukumbi wa AT&T Stadium mjini Arlington, Texas nchini Marekani.
Awali pambano hilo lilikumbwa na misukosuko baada ya kuhairishwa kutoka Julai 20 mwaka 2024 hadi November 15 baada ya Tyson kupata tatizo la kiafya na Daktari wake kumshauri kusitisha mazoezi mazito kwa muda na alifanya hivyo.
Tyson kabla ya kurejea katika pambano hilo alishapoteza dhidi ya Kevin McBride kwa ‘TKO’ katika raundi ya sita, kwenye ukumbi wa MCI Center ambao kwa sasa unajulikana kama Capital One Arena.
Katika pambano hilo la kurejea kwa Tyson, pambano la daraja la uzito wa juu ‘Heavyweight Division fight’ raundi nane, dakika mbili, wote wawili walivalia Gloves za aina ya 14oz kwa ajili ya usalama wao na sio 10oz ambazo mabondia wa kulipwa huzivaa.
Hata hivyo kwa kuwa ni pambano rasmi la ngumi za kulipwa, ‘Knock Down’ na ‘Knock Out’ ziliruhusiwa bila kikinga kichwa ‘Headgear’ na matokeo ya pambano hilo yameingizwa katika rekodi rasmi za ngumi za kulipwa Duniani.
Pambano hilo la 59 kwa Mike Tyson tangu alivyoanza kucheza ngumi na ni pambano lake la saba kupoteza.
Kwa upande wa mpinzani wake Jake Paul limekuwa pambano lake la 12, kushinda na angepoteza lingekuwa pambano lake la pili.
Katika pambano hilo, Jake Paul amemshinda Mike Tyson
Kwa kumpiga ngumi 78 dhidi ya 18 za Tyson katika shindano hilo la dakika 16 kwa uamuzi wa majaji wote mbele ya mashabiki 70,000 Texas na limefuatiliwa na mamilioni ya watu waliotazama pambano hilo kupitia Netflix ambapo Paul alimshinda kwa majaji wote wakitoa alama 80–72, 79–73 na 79–73.
Baada ya pambano hilo Tyson alisema hakutaka kuthibitisha chochote kwa yeyote na anafuraha kucheza pambano hilo huku akimsifu mpinzani wake kwa uhodari wake.
Michael Tyson aliyezaliwa Juni 30, 1966 ni mwanamasumbwi wa wa zamani wa Marekani ambaye alishindana kutoka 1985 hadi 2005 katika ngumi a ushindani. Alipewa jina la utani ‘Iron Mike’ lakini pia anafahamika kama mmoja wa mabondia wa uzani wa juu zaidi wa wakati wote kuwahi kutokea, alitamba kama bingwa asiyepigwa duniani wa uzani wa juu kutoka 1987 hadi 1990.
Tyson ameweka rekodi ya bondia mdogo zaidi duniani kuwahi kushinda taji la uzani wa juu akiwa na umri wa miaka 20, miezi 4 na siku 22 tu. Pia Tyson ndiye bondia wa kwanza wa uzito wa juu kushikilia kwa wakati mmoja mataji ya Chama cha Ndondi cha Dunia (WBA), Baraza la Ndondi Ulimwenguni (WBC) na Shirikisho la Ndondi la Kimataifa (IBF
Licha ya Tyson kupoteza ubingwa wa uzito wa juu usiopingika alipopigwa na Buster Douglas, mwaka 1992, alipatikana na hatia ya ubakaji na akahukumiwa miaka sita jela. Aliachiliwa Baada ya kuachiliwa huru mwaka wa 1995 kwa msamaha baada ya kutumikia miaka mitatu, alirejea katika ngumi na kurejesha mataji ya WBA na WBC mwaka 1996 na kujiunga na Floyd Patterson, Muhammad Ali, Tim Witherspoon, Evander Holyfield na George Foreman kama wanaume pekee katika historia ya ngumi kupata tena, ubingwa wa uzito wa juu baada ya kuupoteza.
Baada ya kupokonywa taji la WBC mwaka huo huo, Tyson alijaribu kutetea taji la WBA dhidi ya Evander Holyfield, ambaye alikuwa kwenye pambano la nne la kurejea kwake mwenyewe. Holyfield alikuwa amestaafu mwaka wa 1994 kufuatia kupoteza ubingwa wake kwa Michael Moorer.
Mnamo Novemba 9, 1996, huko Las Vegas, Nevada, Tyson alipambana na Holyfield katika pambano la ubingwa. Katika hali ya kushangaza, Holyfield, ambaye hakupewa nafasi yoyote ya kushinda na wachambuzi wengi, alimshinda Tyson kwa TKO wakati mwamuzi Mitch Halpern aliposimamisha pambano katika raundi ya kumi na moja. Holyfield amekuwa bondia wa pili kushinda mkanda wa ubingwa wa uzito wa juu mara tatu.
Pambano hilo liliingiza dola milioni 100. Tyson alipokea dola milioni 30 na Holyfield $35 milioni.
Mnamo 1996, Lennox Lewis alikataa dhamana ya $ 13.5 milioni kupigana na Tyson. Huu ungekuwa mkoba wa juu zaidi wa Lewis hadi leo. Kisha Lewis alikubali dola milioni 4 kutoka kwa Don King kujitenga na kumruhusu Tyson kupigana na Bruce Seldon kwa dola milioni 30 zilizotarajiwa badala yake kwa nia kwamba kama Tyson angemshinda Seldon, angepigana na Lewis baadaye. Tyson aliongeza mkanda wa WBA kwa kumshinda bingwa Seldon katika raundi ya kwanza mwezi Septemba mwaka huo.
Tyson ameonekana Katika filamu na televisheni, alionekana kwenye Rocky Balboa (2006), The Hangover (2009), Mike Tyson Mysteries (2014–2020), Ip Man 3 (2015), na Kickboxer: Retaliation (2018). Alionekana kama bosi wa mwisho katika mchezo wa video wa Mike Tyson’s Punch-Out!! (1987). Ushujaa wake wa kibinafsi na kitaaluma ulisimuliwa katika filamu ya hali halisi ya Tyson, iliyoonyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Filamu la Cannes mnamo 2008. Kumbukumbu zake Undisputed Truth (2013) na Iron Ambition: My Life with Cus D’Amato (2017) ziliandikwa na Larry Sloman.
Michael ‘Iron’ Tyson amezaliwa katika Fort Greene, Brooklyn, New York City, Juni 30, 1966. Tyson anaishi Seven Hills, Nevada. Ameoa mara tatu, na ana watoto saba, mmoja amefariki, wanawake watatu; pamoja na watoto wake wa kumzaa, Tyson anajumuisha binti mkubwa wa mke wake wa pili kama mmoja wa watoto wake.
Pia Ana kaka mkubwa aitwaye Rodney aliyezaliwa karibia 1961 na alikuwa na dada mkubwa aitwaye Denise, ambaye alikufa kwa mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 24 mnamo Februari 1990. Mamake Tyson, mzaliwa wa Charlottesville, Virginia, Baba mzazi wa Tyson anaelezwa ni Purcell Tyson’ aliyekuwa dereva wa teksi lakini mtu ambaye Tyson alimjua kama babake alikuwa pimp aitwaye Jimmy Kirkpatrick. Kirkpatrick alitoka Grier Town, North Carolina (eneo lenye watu weusi wengi ambalo lilitwaliwa na jiji la Charlotte).
Tyson alinaswa mara kwa mara akifanya uhalifu mdogo na kupigana na wale ambao walidhihaki sauti yake. Hakuendelea na shule aliishia katika Shule ya Tryon huko Johnstown, New York.
Uwezo wa kuibuka wa ndondi wa Tyson uligunduliwa hapo na Bobby Stewart, mshauri wa kituo cha mahabusu ya watoto na bondia wa zamani. Stewart alimchukulia Tyson kuwa mpiganaji bora na alimfundisha kwa miezi michache kabla ya kumtambulisha kwa meneja wa ndondi na mkufunzi Cus D’Amato anayetambuliwa na Tyson kama baba mlezi.
Mama yake Tyson alifariki akiwa na umri wa miaka 16, na kumwacha chini ya uangalizi wa D’Amato, ambaye angekuwa mlezi wake halali. Tyson baadaye alisema, hajawahi kuona mama yake akifurahi na yeye wala kujivunia kwa chochote alichofanya, alimjua tu kama mtoto wa mitaani, hakujali chochote uhusu yeye na wala hakuwahi kupata nafasi ya kuzungumza naye au kujua chocote kuhusu yeye.
Kwenye mafanikio hapakosi changamoto Tyson nje ya ulingo nayo yalianza kujitokeza. Ndoa yake na Robin Givens ilikuwa ikielekea talaka, na mkataba wake wa baadaye ulikuwa ukipiganiwa na Don King na Bill Cayton. Mwishoni mwa 1988, Tyson aliondoka na meneja Bill Cayton na kumfukuza mkufunzi wa muda mrefu Kevin Rooney, mtu ambaye wengi walimsifu kwa kuheshimu ufundi wa Tyson baada ya kifo cha D’Amato.
Februari 22, 2003, Tyson alimshinda mpinzani wake Clifford Etienne kwa sekunde 49 katika raundi ya kwanza. Hatimaye huu ukawa ushindi wake wa mwisho ulingoni.
Mnamo Agosti 2003, baada ya miaka mingi ya matatizo ya kifedha, hatimaye Tyson aliwasilisha kesi ya kufilisika. Tyson alipata zaidi ya $30 milioni kwa mapambano yake kadhaa na $300 milioni wakati wa kazi yake. Wakati huo, vyombo vya habari viliripoti kwamba alikuwa na deni la takriban dola milioni 23.
Baada ya hapo alitangaza kufanya mfululizo wa maonesho, na kuyaita Tyson’s World Tour. Kwa pambano lake la kwanza, Tyson alirejea ulingoni mwaka wa 2006 kwa maonesho ya raundi nne dhidi ya mtunzi wa uzito wa juu Corey Sanders huko Youngstown, Ohio. Tyson alicheza chini ya kiwango kiasi kwamba pambano hilo lilipokelewa vibaya na mashabiki na mapambano mengine