FeaturedLigi Daraja La Kwanza

Kaa nyuma nitakufungua – Gamondi

Kaa nyuma nitakufungua – Gamondi

MFUMO wa kuzuia (park bus) na kushambulia kwa kushtukiza (counter attack) haujawahi kumsumbua kocha wa Yanga Miguel Gamondi akiamini ana wachezaji wazuri wakuwafungua mabeki wa timu pinzani.

Gamondi amezungumza hayo kuelekea mchezo wa robo fainali wa CRDB Federation Cup  dhidi ya Tabora United.

“Tumecheza na timu nyingi ambazo zinakaa nyuma na kupoteza muda lakini najua uwezo wa wachezaji wangu, tupo tayari kucheza katika mazingira yoyote,”amesema Gamondi.

Utengenezaji nafasi na kuzitumia kwa ufanisi ni kitu pekee Gamondi anahitaji wachezaji wake watumie kwa umakini ili kuvuka kwenda nusu fainali.

Gamondi amesema wachezaji wa timu hiyo wana njaa na kiu ya mafanikio, pia amefurahishwa zaidi na mazoezi ya jana kuelekea mchezo huo.

Related Articles

Back to top button