Yanga yamnyima usingizi Ibenge

KOCHA Mkuu wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibengé ameweka wazi kuwa mechi ya Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Yanga haitakuwa rahisi kwa sababu Yanga watahitaji kulipa kisasi baada ya kuwaondoa katika mashindano hayoa misimu miwili iliyopita.
Yanga wanakutana kwa mara nyingine dhidi ya Al Hilal ya Sudan kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa kundi moja wakiwa na timu ya TP Mazembe (DR Congo) na MC Alger ya Algeria.
Ibenge amesema mchezo wao na Yanga hautakuwa rahisi kwa sababu wamewahi kuwaondoa katika mashindano hayo na watacheza kwa tahadhari kubwa.
“Yanga wana timu nzuri, wamefanya vizuri ndani ya misimu hii ndani n na katika michuano ya kimataifa, tunawaheshimu wapinzani wetu, tulikuwa nao kundi moja na tunahitaji kufanya vizuri na kusonga mbele ya mashindano,” amesema kocha huyo.
Ikumbukwe kuwa Al Hilal ya nchini Sudan iliwaondoka Yanga msimu ambao ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) Yanga ilitolewa katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
Mchezo wa kwanza ambao ulipigwa kwa Mkapa Oktoba 8 mwaka 2022 uliisha kwa sare ya 1-1 na mchezo wa marudiano ambao uliofanyika Sudan Oktoba 16 Yanga ilifungwa bao moja
Msimu huu wa 2024/2025 wa CAFCL Yanga na Al Hilal zimepangwa kundi A,wawili hao watacheza mchezo wa kwanza kati ya Novemba 26 au 27 hapa Tanzania.