Muziki

Youtube kumfanyia sherehe Burna Boy live miaka 5 ya ‘African Giant’

LAGOS: YouTube Music Nights leo itaendesha tamasha maalum litalorushwa mubashara likimshirikisha mwanamuziki nyota wa Nigeria Burna Boy katika kusherehekea kumbukumbu ya miaka mitano ya albamu yake iliyotazamwa zaidi ya, ‘African Giant’.

Tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika leo Julai 26, 2024, litarushwa moja kwa moja kwenye chaneli ya YouTube ya Burna Boy na litaruhusu mashabiki kote ulimwenguni kujiunga na sherehe hizo.

Mkuu wa Muziki wa YouTube barani Afrika, Addy Awofisayo katika chapisho lake alisema; “Tunafuraha kuwasilisha Burna Boy kwenye YouTube Music Nights, kusherehekea kumbukumbu yake ya miaka 5 ya albamu bora kabisa, African Giant.”

Akielezea furaha yake katika chapisho kwenye ukurasa wake rasmi, Burna Boy alisema; “Kuadhimisha miaka 5 ya ‘African Giant’ kwa onyesho maalum jijini London na kuungwa mkono na YouTube Music, kumekuwa tukio la kushangaza kwake.

“Albamu hii ina nafasi ya pekee moyoni mwangu kwani inawakilisha wakati muhimu katika kazi yangu na kauli yenye nguvu ya fahari ya Kiafrika.” Alieleza Burna Boy.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button