Ligi KuuNyumbani

Yanga yaifuata Mtibwa

MSAFARA wa wachezaji 19, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo umeondoka Dar Es Salaam leo mchana kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga itakuwa wageni wa Mtibwa, Disemba 31,2022, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Manungu Complex uliopo Manungu.

Taarifa ya Yanga imewataja wachezaji waliosafiri kuwa ni Djigui Diarra, Erick Johora, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, Yanick Bangala, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Gael Bigirimana na Zawadi Mauya.

Wengine ni Salum Abubakar, Jesus Moloko, Farid Mussa, Dickson Ambundo, David Bryson, Tuisila Kisinda, Yusuph Athumani, Clement Mzize, Stephanie Aziz Ki na Fiston Mayele.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button