Ligi Kuu

Yanga yaifungia kazi Mashujaa

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na kocha Hamdi Miloud, kimewasili Kigoma salama na kipo tayari kusaka alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa FC, utakaochezwa Jumapili Februari 23, Uwanja wa Lake Tanganyika.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kikosi cha wachezaji wote akiwemo Stephen Aziz Ki ambaye  ni bwana harusi wamefika salama na wamepokelewa vizuri na mashabiki wa Yanga Kigoma na wapo tayari kwa ajili ya kutafuta alama tatu katika mchezo huo muhimu.

“Hizi ni mechi za lala salama hutakiwi kupoteza pointi na malengo yetu ya msimu huu tumekuja kutafuta pointi tatu dhidi ya Mashujaa FC, tunatambua hautakuwa mchezo rahisi lakini tumejipanga vizuri,” amesema.

Kamwe amesema wanaiheshimu Mashujaa FC,  timu ngumu iliwasumbua mzunguko wa kwanza wakiwa nyumbani katika Uwanja wa KMC kwa kushinda bao 3-2.

“Wachezaji wote waliopo kwenye mipango ya kocha Miloud wapo tayari kwa mchezo na tunatarajia kupata matokeo mazuri kulingana na maandalizi yaliyofanyika chini ya kocha wetu ,” amesema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button