Tetesi

Yanga, Simba wapigana vikumbo kwa Mwamnyeto

DAR ES SALAAM: WAKATI Yanga wakipambana kumbakiza beki wao, Bakari Mwamnyeto, Simba wameingilia kati dili hilo baada ya kufanya mazungumzo na nyota huyo kwa ajili ya kupata saini yake kwa msimu ujao wa mashindano.

Mkataba wa beki huyo umefika tamati msimu uliomalizika baada ya kuitumikia Yanga miaka miwili na waajiri wake hao wapo katika mchakato wa kumbakiza nyota huyo ndani ya viunga vya Jangwani.

Simba nao wameanza kuwaingilia kati baada ya kuweka dau kwa beki huyo ambaye ameweka wazi kuwa klabu zote zimekuwa zikifanya mazungumzo na meneja anayemsimamia.

Akizungumza na Spotileo, Mwamnyeto amesema sasa mchezaji huru, mkataba wake na Yanga umefika tamati mwishoni mwa msimu na kuongeza kuwa mazungumzo yanaendelea.

Amesema anawapa kipaumbele waajiri wake kwanza licha ya Simba kuweka mezani ofa yao kuhitaji huduma ya beki huyo kwa ajili ya kuimarisha safu ya Ulinzi.

“Ni kweli mkataba wangu na Yanga umetamatika, ofa iliyopo mezani ikiwemo waajiriwa wangu hao lakini pia Simba wanazungumza na meneja wangu. Tunachoangalia zaidi ni maslahi kazi ni popote tu nafanya,” anasema beki huyo.

Msimu wa 2019\20 Mwamnyeto alitokea Coastal Union na kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao umefikia tamati msimu huu wa mshindano.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button