Africa

Yanga mguu sawa Rwanda

KLABU ya Yanga itaondoka nchini Septemba 14 kwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kwanza raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan Septemba 16.

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Tutakuwa na mabasi rasmi ambayo uongozi wa Young Africans umeendaa. Kila ambaye anahitaji kwenda atahitajika kutoa kiasi cha tsh. 150,000 ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi,”amesema Kamwe.

Kamwe amesema kabla ya timu hiyo kuondoka inatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki Septemba 10.

Kauli mbiu ya Yanga kuelekea mchezo huo ni ‘𝐁𝐔𝐑𝐔𝐃𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐉𝐄 𝐍𝐃𝐀𝐍𝐈.’

 

Related Articles

Back to top button