Ligi Kuu

Yanga kitu gani?

Wote wamepigwa!

DAR ES SALAAM: TIMU ya Azam FC imekusanya alama zote tatu baada ya kuinyuka Yanga bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Bao la Azam FC limefungwa na DJibril kipindi cha kwanza cha mchezo na likadumu hadi dakika 90 za mchezo. kwenye mchezo huo mlinzi kinara wa Yanga Ibrahim Bacca alilimwa kadi nyekundu dakika ya 23 ya mchezo baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji Nassor Saadun.

Matokeo hayo ya leo yanamaanisha kuwa kwasasa hakuna timu ambayo haijapoteza mchezo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwani Yanga ndio walikuwa wamesalia hawajapoteza mchezo lakini sasa wameungana na timu nyingine 15 za ligi kuu kuonja maumivu ya kipigo.

Katika hatua nyingine Azam fc imekuwa timu ya kwanza kuzigusa nyavu za Yanga baada ya ushindi wa leo.

Matokeo hayo yameifanya Azam Fc kufikisha pointi 21 kwenye msimamo wa ligi lakini wanasalia katika nafasi ya nne huku Yanga wakisalia kileleni na pointi 24 juu ya Simba na Singida Black Stars.

Related Articles

Back to top button