Yanga, GSM, CCBRT kuwatibu watoto 400

DAR ES SALAAM:YANGA kwa kushirikiana na GSM Foundation na Hospitali ya CCBRT wameingia makubaliano maalumu ya kutibu watoto 400 ambao wamezaliwa na changamoto ya miguu kifundo inayosababisha kushindwa kutembea.
Wakizungumza Dar es Salaam leo wakati wa utiaji saini, Mkurugenzi wa GSM Foundation Faith Gugu amesema mguu kifundo umekuwa ugonjwa ambao umeathiri watoto wengi kimwili lakini vile vile kisaikolojia na wengine wanabaguliwa kutokana na ulemavu huu.
“Tulianza mazungumzo toka mwaka jana ambapo walileta maombi kwetu kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye mguu kifundo. Kwa kushirikiana na Yanga tukaamua kuchangisha fedha,” amesema.
Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi ambaye pia aliongeza kuwa ni neema kubwa kuona GSM Foundation na Yanga wamejitokeza kuwasaidia na kuhimiza watanzania wengine kuwaunga mkono katika mradi huo.
Amesema serikali chini ya Rais Samia imejitahidi kipiga hatua kuhakikisha kuwa kuna maboresho makubwa katika sekta ya afya.