Filamu

Will Smith apewa mtaa West Philadelphia

PHILADELPHIA: MUONGOZAJI na mcheza filamu Will Smith amekabidhiwa mtaa wenye barabara yenye jina lake katika mji aliozaliwa na kukulia wa West Philadelphia ikiwa ni heshima kubwa kwake.

Meya wa jiji hilo, Cherelle Parker, pamoja na viongozi wengine, walisherehekea na muigizaji huyo aliyeshinda tuzo ya Oscar na mwanamuziki aliyeshinda Grammy nyingi kupitia wimbo wa ‘Summertime,’ ‘Men In Black,’ na ‘Gettin’ Jiggy Wit It.’

Eneo lilpowekwa jina la staa huyo ni sehemu ya 59th ya Mtaa karibu na shule ya sekondari aliyosoma.

Katika sherehe hiyo, Smith alitoa shukrani nyingi kwa mji wake, akisema, “Philly, nakupenda. Mimi ni wako. Wewe ni wangu.” Alitafakari juu ya malezi yake, akiwapa wazazi wake sifa kwa kumtia ndani maadili ya bidii na elimu.

“Hakuna mtu anayepata maisha kirahisi. Hilo lilikuwa mojawapo ya mambo ambayo mitaa hii ya Philadelphia ilinifundisha: kwamba hakuna bure il ani kwa kufanya kazi kwa bidii.”

Huko Philadelphia alikopewa urithi wa mtaa uliopewa jina kwa heshima yake, Will Smith ndiye kielelezo cha kufuatilia ndoto za mtu wengi katika mtaa huo na duniani kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button