Burudani

Wasanii kuvuna mamilioni tamasha la Samia

DAR ES SALAAM: WASANII wa muziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Samia Serengeti April 26, mwaka huu kwenye Viwanja vya Tanganyika Peckers wanatarajiwa kuvuna mamilioni ya fedha.

Hiyo ni kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Kedmon Mapana aliyesema kazi yao ni kuwatafutia wasanii masoko wapate maokoto kupitia tamasha hilo.

Akizungumza Dar es Salaam Dk Mapana amesema tamasha hilo lililoko chini ya serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Basata litawanufaisha wasanii mbalimbali fedha lakini pia, wasanii watashamiri kitaifa na kimataifa.

“Wasanii kaeni mkao wa kula, tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara yetu na sisi kama Basata ni kuwatafutia masoko wasanii, Samia inakuja kivingine. Wasanii watapata maokoto,”amesema.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gerson Msigwa ameomba mashabiki mbalimbali pande zote za Tanzania kujitokeza siku hiyo kufurahi Pamoja.

Amesema wasanii wote wakubwa Tanzania watakuwepo kutoa burudani. Miongoni walioorodheshwa kwenye akaunti ya mtandao wa wizara na Basata wamo Ali Salehe ‘Alikiba’, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Zuhura Othman ‘Zuchu’, Faustina Charles ‘Nandy’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na wengine.

Msigwa amesema pia, kutakuwa na mazoezi ya Jogging siku hiyo saa 12:00 asubuhi.

Related Articles

Back to top button