Ligi KuuNyumbani

Ushindi umetuongezea nguvu kusaka ubingwa-Ongala

KOCHA Msaidizi wa Azam, Kally Ongala amesema pointi tatu iizopata timu hiyo dhidi ya Mbeya City, zimeiongezea nguvu klabu kupambana kusaka ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema haikuwa mechi rahisi kwao kutokana na Mbeya City kuleta upinzani.

“Wachezaji walikuwa makini sana kwa kujituma na kufuata kile tulichowaelekeza ingawa Mbeya City walikuwa wagumu.Walitushambulia sana lakini walinzi wetu walikuwa imara,” amesema Kally.

Mshambuliaji wa Azam, Rodgers Kola

Kocha huyo pia amezungumzia kadi nyekundu ambayo ameoneshwa mshambuliaji wake Rodgars Kola, akisema ilikuwa bahati mbaya na hakukusudia.

“Ni kweli alistaili kadi nyekundu lakini ilikuwa ni tukio ambalo hakukusudia na siyo tabia ya Kola,” amesema Kally.

Related Articles

Back to top button