Muziki

Tyla ang’ara tuzo za VMA 2024, aweka rekodi yake

NEW YORK:* MWIMBAJI wa Afrika Kusini Tyla ameweka historia kwenye Tuzo za Muziki za Video za MTV 2024, zilizotolewa UBS Arena huko Elmont, New York, nchini Marekani jana usiku wa Septemba 11.

Mkali huyo mzaliwa wa Johannesburg alishinda tuzo ya Best Afrobeats kwa wimbo wake wa “Water,” na kuweka rekodi yake mpya ya kuwa msanii wa kwanza wa kike wa Kiafrika na msanii wa kwanza wa Afrika Kusini kutwaa tuzo hizo za VMA.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye amejizolea tuzo mbalimbali katika mwaka huu wa 2024 zikiwemo tuzo za Grammys, BET, Billboard, na kipengele cha jalada katika toleo la Oktoba la Elle Magazine, alivyopanda jukwaani kupokea tuzo yake aliwashukuru watu wote waliosababisha mafanikio yake kwa mwaka huu.

“Asante, MTV, timu yangu, Mungu, na kila mtu. Wakati huu ni kumbukumbu kwa Afrika. Mafanikio ya kimataifa yanadhihirisha uwezo wa muziki wa Kiafrika kwenye jukwaa la dunia,” Tyla alisema.

Aliongeza, “Ingawa ni heshima kushinda Best Afrobeats, nataka kuangazia kwamba muziki wa Kiafrika una aina nyingi sana ingawa Afrobeats imefungua milango mingi, lakini tunapaswa kusherehekea wigo kamili wa muziki wa Kiafrika. Ninawakilisha amapiano kutoka Afrika Kusini na utamaduni wangu. Pongezi kubwa kwa wasanii wenzangu wote wa Afrobeats akiwemo Tems, Ayra Starr, Lojay, Rema, Wizkid, Burna Boy na wengine wengi, sote tunang’aa pamoja. Afrika na ulimwengu!”

Katika tuzo hiyo Tyla alishinda nyimbo za wasanii mbalimbali akiwemo Ayra Starr aliomshirikisha Giveon, Burna Boy, Chris Brown akimshirikisha Davido, Lojay, Tems na Usher aliomshirikisha Pheelz.

Mbali na ushindi wake wa Best Afrobeats, pia aliteuliwa kuwa Best R&B kwa wimbo wake wa “Water” na Msanii Bora Mpya. Tuzo nyingine ni Pamoja na Tuzo ya R&B Bora iliyinyakuliwa na SZA kupitia wimbo wake wa “Snooze,” na Chappell Roan ndiye aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora Mpya.

Related Articles

Back to top button