Muziki

Tyla aandika historia Grammy

Awashinda Burna Boy, Davido na Ayra Starr

LOS ANGELES: MSANII chipukizi wa muziki wa pop kutoka Afrika Kusini, Tyla, ameandika historia mpya katika tuzo za Grammy 2025 baada ya kushinda tuzo yake ya pili, akiwashinda mastaa wakubwa wa Afrika akiwemo Burna Boy, Davido, Ayra Starr pamoja na Eddy Kenzo wa Uganda.

Tyla mwenye miaka 24 alitwaa tuzo ya Best African Music Performance kupitia wimbo wake maarufu wa ‘Push 2 Start’, uliopigiwa kura nyingi na wajumbe wa Recording Academy kutokana na mvuto wake mkubwa duniani.

Ushindi huo unaifanya Tyla kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo, baada ya mwaka 2024 kutwaa tuzo hiyohiyo kupitia wimbo ‘Water’, uliompa umaarufu wa kimataifa na kumtambulisha rasmi kama sauti mpya yenye nguvu kutoka Afrika.

Kipengele hicho kinalenga kuonesha ukuaji wa muziki wa Afrika katika jukwaa la kimataifa, lakini ni wimbo wa Tyla uliovutia zaidi na hatimaye kumpa ushindi.

Ushindi huo unaonesha uwezo mkubwa wa Tyla na namna anavyokubalika na jamii yake Kauli hiyo ilieleza wazi kuwa ushindi wake haukuwa wa binafsi pekee, bali ni ushindi kwa Afrika nzima katika uwakilishi wa muziki duniani.

“…! Najihisi mwenye bahati kubwa kuwa hapa, na ninajivunia sana kuwa Mwafrika. Nafurahia kuona Waafrika wengi zaidi wakifika hapa.”

Related Articles

Back to top button