Africa
Simba mguu sawa Zambia

KIKOSI cha wachezaji 24 wa timu ya Simba kimeondoka mchana huu kwenda Zambia kwa ajili ya mchezo wa kwanza kuwania kufuzu makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos Septemba 16.
Taarifa ya Simba imewataja magolikipa kuwa ni Ally Salum, Hussein Abel na Ayoub Lakred.
Mabeki ni Shomari Kapombe, Davida Kameta Duchu, Israel Mwenda, Mohammed Hussein, Hussein Kazi, Henock Inonga, Che Malone Fondoh na Kennedy Juma.
Viungo ni Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma, Hamis Abdallah, Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama, Willy Onana, Luis Miquissone na Kibu Denis.
Washambuliaji ni Jean Baleke, Moses Phiri, Shabani Chilunda na John Bocco.