AfricaKusini Mwa Afrika
Twiga Stars dimbani leo

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake(Twiga Stars) leo inaanza kutetea taji la Ubingwa wa Vyama vya soka Kusini mwa Afrika(COSAFA) dhidi ya Comoros kwenye uwanja wa Madibaz uliopo jiji la Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Twiga ililitwaa taji hilo katika fainali Oktoba 9, 2021 kwa kuifunga Malawi bao 1-0 ikiwa mgeni mwalikwa.
Mchezo mwingine wa michuano hiyo leo ni kati ya Botswana na Malawi.
Michezo miwili imepigwa Septemba Mosi ambapo Lesotho iliifunga Eswatini mabao 3-0 huku Zambia ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Namibia.
Michuano ya COSAFA 2022 kwa wanawake imefunguliwa Agosti 31.