Kwingineko

“Tunastahili heshima” – Kocha Fluminense

EAST RUTHERFORD, Meneja wa Fluminense raia wa Brazil Renato Portaluppi amesema safari ya kikosi chake hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu inapaswa kuwapa heshima makocha wa wenye asili ya Brazil, baada ya mbio zao kutamatishwa na Chelsea kwa mabao 2-0 usiku wa kuamkia leo.

Mshambuliaji huyo wa zamani, ambaye aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Rio de Janeiro mwaka wa 1995 akiwa mchezaji, ameiwezesha Fluminense kutoka kuwa wapiganiaji wa kushuka daraja na kuwa timu tishio katika kipindi cha miezi mitatu tu kama Kocha.

“Ninatumai sio tu duniani kote lakini pia Brazil, watu wanaweza sasa kuwaangalia makocha wa Brazil kwa jicho tofauti na kuwathamini zaidi,” alisema Portaluppi

“Sina chuki na makocha kutoka sehemu nyingine duniani lakini watu wanawazungumza sana na hawawazingatii sana makocha wa Brazil. Kombe hili la Dunia la Klabu limeruhusu makocha wa Brazil kuonekana katika ‘engo’ nzuri zaidi na ninatumai hilo halitabadilika.” Aliongeza

Portaluppi ambaye ni mkosoaji mkubwa wa makocha wa kigeni ndani ya ligi ya Brazil amesema pia nguvu ya makocha hao iliyoonekana uwanjani itawasha taa ya heshima kwa makocha wazawa wa Brazil na heshima itaenea Duniani kote.

Kombe la Dunia la Klabu limekuwa ‘pepo’ kwa timu za America Kusini kwani wakati mwingine zimetoa matokeo ya kustaajabisha dhidi ya timu vigogo kutoka Ulaya ambako soka kimepiga hatua kubwa. Portaluppi, amewaahidi mashabiki wa Fluminense kuendeleza moto huo kwenye ligi ya nyumbani.

Related Articles

Back to top button