Kwingineko

Nani kumfuata Dortmund fainali UCL?

MCHEZO wa marudiano wa nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mbaingwa ulaya(UCL) kati ya Real Madrid na Bayern Munich unapigwa leo kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu uliopo mji mkuu wa Hispania, Madrid.

Katika mchezo wa kwanza Aprili 30 timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa
Allianz jijini Munich, Ujerumani.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo wa leo atakipiga fainali Juni Mosi, 2024 kwenye uwanja wa Wembley jijini London, England dhidi ya Borussia Dortmund ambayo Mei 7, imeitoa Paris Saint-Germain kwa jumla ya mabao 2-0.

Wakati huo huo mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Europa Conference kati ya Club Brugge na Fiorentina unafanyika leo kwenye uwanja wa Jan Breydel uliopo mji wa Bruges, Ubelgiji.

Fiorentina ilishinda mchezo wa kwanza Mei 2 kwa mabao 3-2 dhidi ya Club Brugge.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button