
BODI ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ya michezo sita ya Ligi hiyo.
Taarifa ya TPLB imesema sababu za maboresho hayo ni baadhi ya timu zinazohusika na michezo hiyo kuwa na wachezaji waliojiunga na timu zao za taifa.
Kwa mujibu wa maboresho hayo mchezo kati ya KMC na Mtibwa Sugar uliokuwa ufanyike Septemba 27, 2022 utachezwa Oktoba 15 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Mchezo kati ya Ruvu Shooting na Coastal Union umesogezwa kutoka Septemba 26 hadi Septemba 29 kwenye uwanja wa Uhuru.
Taarifa imesema mchezo kati ya Polisi Tanzania na Namungo uliopangwa kufanyika Septemba 27 sasa utachezwa Okotba 19 kwatika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Katika maboresho hayo Ihefu na Yanga zitacheza Novemba 29 badala ya Septemba 29 katika uwanja wa Highland Estate uliopo Mbeya.
Aidha bodi ya ligi imesema mchezo kati ya Kagera Sugar na Singida Big Stars uliopangwa kufanyika Septemba 28 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza utachezwa Oktoba 21 katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Maboresho hayo yanaonesha mchezo namba 37 Mbeya City dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika Septemba 28 sasa utachezwa Novemba 23 katika uwanja wa Sokoine uliopo Mbeya.