Nyumbani

Pamba Jiji FC yaipania Ligi Kuu

MWANZA: UONGOZI wa Pamba Jiji FC umeweka wazi kuwa wamekuja kivingine kwa kuboresha timu hiyo kuanzia benchi la ufundi na usajili wa wachezaji ambao wataleta ushindani mkubwa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Tayari Pamba Jiji FC, imeingia makubalino na aliyekuwa Kocha wa Simba na Tabora United, Goran Kopunivic kukinoa kikosi hicho kilichoifanikiwa kupada ligi kuu baada ya miaka 23.

Akizungamza Spotileo, Ofisa Habari wa timu hiyo, Martin Sawema amesema walianza kuboresha benchi la ufundi kwa kufanikiwa kumpa jukumu la kukinoa kikosi cha Pamba Jiji FC, Goran na wanashirikiana katika suala la usajili.

Amesema wameshaanza kufanya wa usajili baadhi ya wachezaji wapya 10, wakiwemo wa kigeni na wazawa kwa kushirikiana na kocha huyo kuhakikisha wanarejea kivingine kwenye ligi hiyo.

“Kuna wachezaji tumewasajili kulingana na mahitaji ya timu hiyo kwa kushirikiana na kocha Goran kwa mapendekezo yake, tunafanya usajili mzuri na hatutakuwa wanyonge hasa kwa hizi klabu kubwa za Kariakoo, Simba na Yanga,” amesema Ofisa habari huyo.

Amesema wako makini kwa kusaidia na baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Said Mtanda anaendelea kuwezesha timu hiyo katika mambo mbalimbali kuhakikisha Pamba Jiji FC, inaleta ushindani ligi kuu.

“Usajili unaendelea kufanyika na kila kitu kinaenda vizuri na muda utakapowadia tutaweka wazi tumemsajili nani na kutoka taifa, tunatarajia kuingia kambini mapemba Julai, mwaka huu na kambi tutaweka Morogoro,” amesema Sawema.

Related Articles

Back to top button