Tetesi za usajili

NIA ya Liverpool kumbakisha Mohamed Salah itajaribiwa na ofa ya pauni milioni 129 sawa shilingi bilioni 395 ya klabu ya Al-Ittihad inayoshiriki Ligi ya Kulipwa ya Saudi Arabia.(CBS)
Bayern Munich ina nia kumsajili Scott McTominay kwa mkopo ambapo hatua hiyo itaruhusu Ryan Gravenberch kujiunga na Manchester United kwa mkopo .(Bild)
Manchester United inaweza kuanza mpango wa kuhitaji huduma ya Pierre-Emile Hojbjerg wa Tottenham wakati juhudi za kusaka kiungo zikiendelea.(Telegraph)
Chelsea inafikiria kumnunua kiungo mshambuliaji Emile Smith Rowe wa Arsenal pamoja na Raphinha na Ferran Torres wa Barcelona.(Mail)
Rais wa Real Madrid amekuwa akipokea ofa kutoka kwa mawakala, vilabu na wapatanishi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji baada ya kuthibitika kuwa majeraha aliyepata Vinicius Junior ni makubwa. (Marca)
Tottenham haiko tayari kuongeza muda mwingine wa mkopo kwa Giovani Lo Celso ambaye ameonekana kuwindwa na Barcelona. Uhamisho wa kudumu unafikiriwa kuwa chaguo pekee. (Mundo Deportivo)
Arsenal inamfuatilia beki wa Crystal Palace, Marc Guehi huku kukiwa na utata kuhusu hatma ya Gabriel Magalhaes kunako Emirates.(Mail)
Manchester United pia imetuma ombi kuhusu beki wa kushoto wa Brentford, Rico Henry kama uwezekano wa mbadala wa majeruhi, Luke Shaw.(Mail)
Brennan Johnson angependa kujiunga na Tottenham badala ya Brentford na uhamisho wa ada ya pauni milioni 50 kutoka Nottengham Forest kwenda Kaskazini ya London unakaribia.(The Times)