Muziki

Taylor Swift apiga shoo ya mwisho

Avunja rekodi ya Elton John

CANADA: MWANAMUZIKI anayeshikilia namba moja kwa utajiri kwa wanamuziki wa kike duniani, Taylor Swift amefanya onesho la mwisho la ziara yake ya ‘Eras’ iliyovunja rekodi baada ya kuingiza pesa nyingi mno katika historia ya muziki wake.

Onesho hilo limefanyika wikiendi hii huko Vancouver nchini Canada, onesho hilo lililokuwa onesho la Era 149, kufuatia vituo kutoka Buenos Aires hadi Paris na Tokyo, limekuwa tukio kubwa lililoenea duniani kote likianzia katika jimbo la Arizona, Marekani Machi 17, 2023.

Gazeti la Vancouver Sun limeandika kwamba Swift ameonekana jukwaani katika uwanja uliouzwa nje wa BC Place muda mfupi kabla ya saa 8:00 (0400 GMT) na kuuambia umati kwamba amehisi kuwa Vancouver umekuwa usiku wake mzuri mno.

Hata hivyo kambi ya Swift haijatoa hadharani idadi ya mapato ya tikiti kwa ziara hiyo lakini jarida la biashara linalotajwa sana la Pollstar limekadiria idadi hiyo kuwa ni zaidi ya dola bilioni 2.

Kwa hali hiyo imevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Elton John ya ‘Farewell Yellow Brick Road Tour’ ambayo iliuza wastani wa dola 939 milioni katika maonesho 328 yaliyoenea kwa miaka mitano.

Uwepo wa Swift katika miji na kumbi mbalimbali umeongeza uchumi wa ndani wa maeneo hayo. Kituo chake cha pili cha ziara kilikuwa Toronto, ambapo alifanya maonesho sita ndani ya wikendi mbili na alizalisha dola milioni 282 na dola za ziada milioni 199.

Wakaguzi wamemsifu Swift kwa ustahimilivu katika maonesho yake ndiyo maana amefanikiwa kumaliza bila shaka yoyote ingawa katika tamasha la Vienna majira ya joto wakati maonesho matatu yalifutwa baada ya mamlaka kumkamata mtu anayehusishwa na njama za kufanya mashambulizi.

Pia kuna shabiki alikufa kutokana na uchovu wa joto wakati wa onesho lake huko Brazil katika jiji la Rio de Janeiro mnamo Novemba mwaka jana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button