Burudani

TASIMA na mikakati ya Singeli

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Muziki wa Singeli Tanzania (TASIMA) kinatarajia kuwajengea uwezo wasanii wa muziki huo na kuufanya kuwa muziki wakipekee zaidi utakaotikisa anga za Kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa chama hicho, Masudi Kandoro ‘Kandoro Baba’ amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi kuwa Muziki wa Singeli unatakiwa kupewa kipaumbele.

“Tunaunga mkono kauli hizo tofauti za viongozi waoutazamia muziki wa singeli na kuona kuwa ni muziki utakao tubadilisha na kututangaza zaidi kimataifa.

“Lengo ni kuwabadilisha wasanii kuwa na matendo mazuri, muonekano pamoja na kuwapatia elimu itakayowapa uewelewa na kujua vitu ikiwemo na kujifunza lugha za watu wengine zitakazowafanya kuwasiliana vizuri na mashabiki wao.

Aidha ameongeza kuwa kumekuwa na wasanii tofauti tofauti wa Kimataifa ambao wamekuwa wakioonesha kufurahia na mziki wa singeli.

“Niwakati wa wasanii kuungana na kututangaza muziki wa pekee utakaopeperusha bendera na kutuletea tuzo za Grammy kwa upekee wake.

“Wasanii kama Snop Dog, Chris Brown wamekuwa wakisapoti muziki wa singeli kwa kuimba muziki huo, ambao ukizingatia unaweza kutuletea tuzo ya grammy nchini ni muziki wa singeli.”amesema Kandoro

“Singeli to the World tuta hakikisha wasanii wanajikita kutangaza vitu vya Kitanzania zaidi kwa kuwashirikisha wasanii mbalimbali kama wabunifu wa ndani pamoja na wachoraji ili kutengeneza kitu kizuri.

Kwa upande wake Samadu Abdallah, ‘Samio love’ amesema kuwa Muziki wa Singeli na kuimba matusi ni jambo la mtu binafsi ili muziki wako uheshimike unapaswa kuwa na maadili.

“Aina ya muziki wa singeli kuimba matusi sio chama bali ni mtu binafsi na kile anachokiimba yeye binafsi itakuwa nafasi ya kutenganisha matusi na kuburudishaji katika kuimba Singeli.

Related Articles

Back to top button