WACHEZAJI 25 wa kikosi cha timu ya taifa ya soka ‘Taifa Stars’ wameondoka leo kwenda Tunis, Tunisia kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) dhidi ya Algeria utakaopigwa Septemba 7.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa 19 May 1956 uliopo eneo la Annaba, Algeria.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche amewataja wachezaji hao kuwa ni Beno Kakolanya, Metacha Mnata, Erick Johora, Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Mzamiru Yassin, Sospeter Bajana, Clement Mzize, Kibu Denis, Himid Mao, Mudadhir Yahaya na Abdul Sulaiman.
Wengine ni Abdulmalik Zakaria, John Bocco, Kenedy Juma, Lameck Lawi, Jonas Mkude, Morice Abraham, Haji Mnoga, Ben Starkie, Saimon Msuva, Novatus Miroshi, Mbwana Samatta na Abdi Banda.




