Africa

Ngorongoro Heroes nao wamo!

DAR ES SALAAM: Mwaka 2024 ulikuwa mtamu kwani Tanzania ilizidi kuwaka ki-soka baada kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, CECAFA U20 na kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) mwakani 2025 ikiiwakilisha CECAFA .

Hayo yanakuja baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya kwenye fainali ya aina yake iliyopigwa Uwanja KMC Complex, Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Haukuwa ushindi mwepesi, kwani Ngorongoro Heroes walilazimika kutoka nyuma na kushinda mchezo huo baada ya kutanguliwa kufungwa bao. Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Kocha mzoefu, Charles Boniface Mkwasa ama muite Master anayesaidiwa na Kally Ongala na Juma Kaseja kama Kocha wa makipa ikazinduka kwa mabao ya mshambuliaji wa Simba, Valentino Mashaka dakika ya 64 na kiungo wa Yanga, Shekhan Khamis dakika ya 82.

Kenya na Tanzania zilikuwa kwenye kundi moja pamoja na Sudan, Rwanda na Djibouti timu hizi kufika fainali inamaanisha kundi lao ndilo lilikuwa kundi gumu au tukae tu chini tukubali kukubaliana kuwa lilikuwa kundi la kifo. Ushindi huu ni kısası cha mchezo wa kwanza wa Kundi A baina ya timu hizo ambapo Kenya walishinda magoli 2-1.

Safari ya mashujaa hawa wa Ngorongoro haikuwa ya mteremko kwani hawakuanza vyema michuano hii baada ya kipigo cha 2-1 dhidi ya kenya kwenye mechi ya ufunguzi walijipapatua na kujipata walishinda mechi mfululizo ikiwemo ule ushindi mnono wa 7-0 dhidi ya Djibouti.

Ikikusanya pointi 7 kwenye kundi na kutinga nusu fainali iliyoanzisha safari ya Ubingwa na kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) mwakani ikiiwakilisha CECAFA pamoja na The Rising Stars timu ya taifa ya vijana ya kenya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button