Ligi Ya Wanawake

Stumai anukia kiatu cha dhahabu

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa JKT Queens Stumai Abdallah ananukia kuchukua kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Wanawake.

Baada ya mchezo wao wa Jana dhidi ya Ceasiaa aliofunga mambo matatu katika ushindi wa mabao matano amefikisha jumla ya mabao 26.

Kuna tofauti ya mabao saba dhidi ya mpinzani wake Jentrix Shikangwa wa Simba Queens mwenye mabao 19.

Katika misimu takribani mitano Stumai licha ya ubora wake hajawahi kuchukua kiatu cha ufungaji bora zaidi amekuwa akingiia kwenye tatu bora.

Huu ni msimu bora kwake kwani kila mechi ametupia isipokuwa za Simba Queens na Yanga princess. Akiwa na mwendelezo mzuri hadi kumaliza mzunguko wa pili basi anaweza kuchukua kiatu cha dhahabu.

Sio tu anaongoza kufunga, ndiye mchezaji mwenye hat trick nyingi msimu huu zinafika tano huku mpinzani wake Shikangwa akiwa na tatu.

Mpaka sasa ameshavunja rekodi yake ya Msimu wa 2023/2024 katika mechi 18 alifunga mabao 19.

Related Articles

Back to top button