Ligi KuuNyumbani

Singida BS yapigwa bei

Uongozi wa Singida Big Stars umethibitisha kuiuza timu hiyo kwa kituo cha kukuza vipaji cha Fountain na sasa timu hiyo itafahamika kwa jina la Singida Fountain Gate.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Singida BS John Kalutu amesema Wana Singida wasiwe na shaka bado wataendelea kuifurahia timu yao.

“Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wetu kwamba uongozi wa Singida Big Stars FC umefanya makubaliano ya kibiashara ya kuuza hisa zake kwa uongozi wa Fountain Gate Academy,”amesema Kalutu.

Amesema makubaliano hayo yameambatana na baadhi ya mabadiliko katika uendeshaji wa klabu kwa upande wa Bodi na Menejimenti.

Singida Big Stars ilibadilishwa jina kutoka Singida United mwaka mmoja uliopita.

Related Articles

Back to top button