Nyumbani
Singida black Stars yamfungia Khalid Aucho

DAR ES SALAAM: KLABU ya Singida Black Stars SC imetangaza kumfungia miezi mitatu kiungo Khalid Aucho kwa kosa la utovu wa nidhamu na kuchelewa kazini.
Aidha, imemsimamisha kazi kipa Amas Obasogie kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuruhusu uchunguzi wa tuhuma zinazohusiana na upangaji wa matokeo.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyolewa leo na Ofisi ya Mtendaji Mkuu, kupitia Kamati ya Nidhamu, imewakumbusha wachezaji kuheshimu taratibu.
“Klabu inawakumbusha wachezaji na watumishi wake wote kuzingatia nidhamu, uwajibikaji na heshima kwa klabu,”imesema taarifa hiyo.




