Riadha

Simbu aweka rekodi mpya Tokyo

mtoto atalelewa na bibi yake

TOKYO: MWANARIADHA wa Tanzania, Alphonce Simbu, ameandika historia kwa kuipa nchi medali ya kwanza ya dhahabu katika mashindano ya dunia ya riadha yanayoendelea jijini Tokyo, Japani.

Simbu aling’ara kwenye mbio hizo kwa kukimbia muda wa saa 2:09:48, na kufanikiwa kumshinda mpinzani wake mkali kutoka Ujerumani, Amanol Petros, kwa tofauti ndogo ya sekunde 0.03 pekee.

Ushindi huu wa kihistoria unaweka jina la Tanzania kwenye ramani ya dunia ya riadha na kumfanya Simbu kuwa shujaa mpya wa michezo hiyo nchini.

Mashindano ya Dunia ya Riadha (World Athletics Championships) ni tukio kubwa la kimataifa linaloandaliwa na Shirikisho la Riadha Duniani (World Athletics) kila baada ya miaka miwili.

Tangu yalipoanzishwa mwaka 1983 mjini Helsinki, Finland, yamekuwa yakikusanya wanariadha bora zaidi duniani kushindana katika mbio mbalimbali kuanzia za mita fupi, ndefu, kuruka na kurusha. Mashindano ya mwaka 2025 yanafanyika jijini Tokyo, Japani, yakihusisha zaidi ya nchi 190 na wanariadha zaidi ya 2,000.

Kwa miaka mingi, Tanzania imekuwa ikishiriki kwenye mashindano haya lakini haijawahi kufanikisha ushindi mkubwa.

Medali nyingi za bara la Afrika zimekuwa zikitwaliwa na wanariadha kutoka Kenya, Ethiopia, Uganda na Afrika Kusini. Ushindi wa Simbu unaweka historia mpya na kufungua ukurasa wa matumaini kwa wanariadha wengine wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button