Africa

Simba yajipanga kurejesha heshima yake

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Steven Barker, amesema bado kuna matumaini kwa kikosi chake katika Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya maumivu ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo uliopita dhidi ya Esperance ya Tunisia mwishoni mwa wiki.

Barker alisema Simba bado ina michezo miwili ya hatua ya makundi, ambayo itatoa fursa ya kujirekebisha, kujifunza kutokana na makosa na kuendelea kupambana kwa ajili ya nembo ya klabu.

“Bado tuna mechi mbili za Ligi ya Mabingwa. Tunapaswa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kupambana kila dakika na kuhakikisha tunaiwakilisha Simba kwa heshima,” alisema Barker.

Wekundu hao wanatarajia kucheza mchezo ujao dhidi ya Petro Atletico ya Angola utakaochezwa Jumamosi nchini Angola.

Simba ni kama imeshapoteza mwelekeo ingawa wao bado wana matumaini kwani inashika mkia kwa pointi moja ilizovuna katika michezo minne yah atua ya makundi. Kinara ni Stade Malien pointi 8, ES Tunisi 6, na Petro 5.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button