Ligi Kuu

Simba yairahisishia kazi Mashujaa

KOCHA Mkuu wa Mashujaa FC, Abdallah Mohammed ‘Bares’, amesema ametumia dakika 90 kuwasoma Azam FC ilipocheza dhidi ya ya Simba, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mashujaa FC walitumia mchezo huo kuwasoma wapinzani wao Azam FC ambao wanatarajia kukutana nao Jumapili, Septemba 29, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema ametumia mechi hiyo kuangalia ubora wa Azam FC, kufanyia kazi uwanja wa mazoezi na kujipanga vizuri kuwakabili wapinzani wao.

“Ni utamaduni wetu kufuatilia mpinzani wenu anapocheza kabla hatujakutana nao, tumeona Azam FC ilipocheza na Simba, tunafanyia kazi kile tulichokiona katika mchezo huo kabla ya kukutana na wapinzani wetu hao,” amesema Bares.

Amesema wanahitaji kupata matokeo katika mchezo huo wanaocheza nyumbani kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya ligi hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button