‘Simba wasibwete, Yanga, GSM zatajwa’

DODOMA: WAZIRI wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema Simba wasibweteke kwa kuwa mafanikio ambayo wanajivunia leo sio mapya kwa Yanga kwani walifika hatua kama hiyo mwaka juzi ambayo kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na uwekezaji uliofanywa na Ghalib Salim Mohamed (GSM).
Amesema GSM ameleta chachu kubwa kwenye mafanikio ya Yanga na kushauri kuwa yanga wanapoandaa ramani ya ujenzi wa uwanja mpya wasisahau kuweka sanamu kubwa ya GSM.
Amehimiza klabu nyingine kuiga hatua hizo za Simba na Yanga kwa manufaa ya soka la Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dk Nchemba amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuboresha sekta ya michezo nchini.
Amesema jitihada hizo zimewezesha nchi kuwa miongoni mwa nchi wenyeji wa mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027.
“Kufanyika kwa mashindano hayo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza na kukuza sekta ya michezo na utalii nchini. Hivyo, nitoe rai kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa hiyo adhimu kwa kuwa ujio wa wageni wakati wa michuano hiyo utahitaji huduma mbalimbali kama malazi, chakula na usafiri,”




