Africa
Simba vs Vipers: Mechi ya kisasi, ubabe

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba leo inashuka dimbani kuivaa Vipers katika mchezo wa marudiano kundi C wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza kwenye uwanja wa St Mary’s Kampala, Uganda ndi wa Simba wa goli 1-0 Februari 25 likifungwa na Henock Inonga.
Michezo mingine ya michuano hiyo leo ni kama ifuatavyo:
Kundi B
Al Hilal Omdurman vs Coton Sport
Kundi C
Horoya vs Raja Casablanca
Kundi D
CR Belouizdad vs El-Merreikh
Zamalek vs Esperance