Africa
Nusu fainali CAFWCL leo
NUSU fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake(CAFWCL) inapigwa leo huko Ivory Coast.
Katika nusu fainali ya kwanza mabingwa watetezi AS far Rabat itaivaa Mamelodi Sundowns katika mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Amadou Gon Coulibaly uliopo mji wa Korhogo.
Ampem Darkoa itakutana na Sporting club Casablanca kwenye uwanja wa Laurent Pokou uliopo mji wa San Pedro.