Ligi KuuNyumbani

Simba vs Azam: Derby ya Mzizima ugenini

MACHO na masikio ya wapenda mpira wa miguu leo yataelekezwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kujua matokeo ya Derby ya Mzizima kati ya Simba na Azam ukiwa mchezo pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba inayonolewa na kocha Abdelhak Benchikha ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 baada ya michezo 12.

Azam chini ya mwalimu Youssouph Dabo ipo nafasi ya 2 ikiwa na pointi 31 baada ya michezo 13.

Takwimu za michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Azam zinaonesha Simba imeshinda mechi 9 kati ya 20 walizocheza dhidi ya Azam tangu Azam ilipopanda Ligi Kuu msimu wa 2008/09.

Azam imeshinda mechi 5.
Mechi 6 zimemalizika kwa sare.

Simba na Azam zimekutana mara 33 katika mashindano yote.

Simba imeshinda mechi 15.
Azam imeshinda mechi 12.
Mechi 7 zimemalizika kwa sare.

Related Articles

Back to top button