Africa
Simba Queens katika mtihani dhidi ya Mamelodi Ladies

TIMU ya soka ya wanawake Simba Queens leo itakuwa na mtihani katika mchezo wa nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns Ladies.
Sundowns Ladies ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo. Mchezo huo utapigwa uwanja wa Prince Moulay Al Hassan katika mji wa Rabat, Morocco.
Sundowns Ladies imeongoza kundi B la michuano hiyo wakati Simba imekuwa mshindi wa pili kundi A.
Nusu fainali nyingine leo itakuwa kati ya ASFAR Club dhidi ya Bayelsa Queens.