Habari Mpya

Kipigo tena Simba mchezo wa kirafiki

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba leo imepokea kipigo cha pili mfululizo katika michezo ya kirafiki baada ya kufungwa bao 1-0 na Association Sportive d’Arta ya Djibouti kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Simba pia ilipoteza mchezo wa kirafiki kwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal Agosti 31 kwenye uwanja wa Al Hilal, Sudan.

Association Sportive d’Arta ilianza ziara ya michezo ya kirafiki nchini kwa kupata kipigo cha mabao 3-0 toka kwa Azam kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button