Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika Dar es Salaam.
Wekundi wa Msimbazi, Simba ni wenyeji wa Wazee wa Mpapaso, Ruvu Shooting katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 11 wakati Ruvu Shooting ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 12.




