RODRI: Haikuwa ndoto yangu kucheza soka
MCHEZAJI@mancity ,Rodrigo Hernández Cascante amesema kucheza mpira wa miguu haikuwa ndoto yake ya awali licha ya kuucheza kwa kiwango cha juu sana katika klabu na timu yake ya taifa ya Hispania.
Katika mahojiano na Joe Hart wa BBC Sport Rodri amesema kuwa alipenda sana kucheza chess. Amesema alipomaliza shule ya sekondari mama yake alimtaka kwenda chuo kikuu ndipo alipogundua kipaji chake na kugundua kuwa na kipaji cha soka.
“Kwangu kucheza soka hakukuwa chaguo la kwanza, nilikuwa mchezaji mzuri wa Chess haikuwa mpaka nilipofika chuo kikuu, wakati nachukua shahada yangu ya kwanza ndio niligundua naweza kucheza soka lakini hii haikunifanya niache masomo nikacheze soka – amesema.
Rodri ambaye bao lake liliipa Manchester City ubingwa wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya alijiunga na klabu hiyo Julai 4 2019 akitokea Atletico Madrid, amekuwa nchezaji muhimu wa kikosi cha Guardiola akijihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha meneja huyo.
Mpaka sasa ameichezea Manchester City michezo 172 ya ligi kuu ya England, akifunga mabao 22 huku akiisaidia kushinda michezo 128 aliyocheza.